UMATI
UNAOZUIA FURSA YAKO
Nehemia 4:1
Utangulizi
Kama somo
linavyojieleza “umati unaozuia fursa”
ni wazi kwamba huu umati upo maalumu kwa ajili ya kuzuia, umekusanyika ili
kuzuia na kupinga jambo Fulani lisifanikiwe, mtu Fulani asifanikiwe kuipokea
fursa yake kwa namna yoyote ile, ni watu walio kusanyana kwa lengo moja la
kuzuia tu hawana jema wala zuli bali jukumu lao kubwa ni kuzuia tu imeandikwa 1Timotheo 5:15 “Kwa maana
wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani”
Kunawatu
wengi wanashindwa kuzitumia fursa zao kwa sababu ya umati ulio mbele yao
unawazuia. Hivyo kuwa ni watu wa kuhangaika na kuteseka mwaka nenda mwaka rudi,
bila mafanikio yoyote hadi kupelekea fursa kuondoka.
N:B yakupasa
kutambua fursa ni kama jua linavyo tembea
Maana ya umati
Umati ni
mkusanyiko wa watu, vitu, katika eneo moja kwa ajili ya lengo Fulani,
inawezekana ikawa ni kikao, kazi, ibaada, tabia, hali, mawazo au mkutano wa aina yeyote,
Kuzuia maana yake nini
Ni kupinga
kitu Fulani au jambo, hali, mawazo, fikira inayoweza kuzuia kitu kisiweze
kufanyika/kutendeka kwa wakati unaofaa/sahihi.
Fursa
N i kitu
chochote maalumu kilicho mbele yako kwa ajili yako, inawezekana ikawa ni
wokovu, biashara, kazi, ndoa au mafanikio yako,
Watu wengi
wanateseka ni kwa sababu kuna watu wanaozuia fursa iliyo mbele yao, kwa kuwaona
au kutokuwaona kwa macho ya kawaida
Vitu au watu
wanaozuia fursa yako wana weza kuwa wanaonekana au hawaonekani, wanaoonekana ni
wale wanaokupinga wazi wazi kwa kila jambo unalolianzisha na wale wasioonekana
wanaweza kukuzuia kwa kutumia njia za kichawi kuzuia usiweze kuipokea fursa
iliyo mbele yako au kuzuia wazi wazi.
Imeandikwa Nehemia 4:1-4 “Lakini ikawa, Sanbalati
aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na
uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.
Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.
Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto? Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.
Tambua ya kwamba wanaozuia fursa
iliyo mbele yako wakawa ni ndugu imeandikwa Mathayo 10:36 “na adui za mtu ni
wale wa nyumbani mwake”
Ø Inawezekana wakawa marafiki ulio nao
Ø Inawezekana wakawa watoto, mume, mke au ndugu mliozaliwa wote
Ø Inawezekana ikawa
jamii/washirika/wafanyakazi/viongozi wenzako
Ø Inawezekana ikawa ufahamu wako
Ø Inawezekana ikawa tabia yako
Ø Inawezekana yakawa mawazo uliyonayo
Ø Inawezekana ikawa muda
Ø Inawezekana ikawa imani yako
Ø Inawezekana ikawa biashara unazozifanya
Ø Inawezekana ikawa kazi unayoifanya
Ø Usipo kuwa makini vinaweza kukuzuia
kukutana na fursa iliyo mbele yako,
Ø Inawezekana vikakuzuia
Ø Kukutana na uponyaji wako
Ø Kuisikia sauti ya Mungu
Ø Kupata msaada
Ø Kufunguliwa
Ø Kukaa miguuni pa Yesu
Ø Kutubu dhambi zako
Ø Kuchelewesha mafanikio yako n.k
Hatua 7 za kuushinda umati unaokuzuia kukutana na fursa iliyo mbele yako
v Kuifahamu kweli juu ya maisha yako imeandikwa Yohana 8:32 ”tena
mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”
v Kuipokea kweli imeandikwa Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
v Mungu awe upande wako imeandikwa warumi 8:31 “Basi, tuseme
nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
v Kumwamini Mungu imeandikwa Waebrania 10:38 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa
imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
v Kuchukua hatua kwa kile unacho
kiamini imeandikwa zaburi 37:23-25 “Hatua
za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka
chini, Bwana humshika mkono na kumtegemeza.
Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa
Wala mzao wake akiomba chakula.
v Kukubali kumsikiliza Mungu ili kupewa
maelekezo na njia ya kufanya ili kuwashinda wanaokuzuia kuiona fursa iliyo
mbele yako, imeandikwa mithali 16:25
“Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za
mauti”
v Kuwa jasiri juu ya kila jambo la haki
Imeandikwa 2Timotheo 1:7 “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na
ya upendo na ya moyo wa kiasi”
HITIMISHO
Watu
wanaangamizwa, wanapata shida ni kwa sababu wamekosa maarifa imeandikwa Hosea 4:6 “Watu wangu
wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami
nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu
wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”
Umati
unaokupinga wewe unaweza ukaja kuwa mateso kwa kizazi chako pia, maombi maalumu
yanafanyika hemani ya kutawanya maadui
imeandikwa zaburi 68:1 “Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika, Nao
wamchukiao huukimbia uso wake”
Barikiwa sana Mtu wa Mungu Tunabarikiwa sana na masomo yako Mungu akubariki sana
ReplyDelete