Tuesday, 13 February 2018

kwanini watu wanakuandama?

                                                     UMATI UNAOZUIA FURSA YAKO
                    Nehemia 4:1
Utangulizi                                                                                    
Kama somo linavyojieleza “umati unaozuia fursa” ni wazi kwamba huu umati upo maalumu kwa ajili ya kuzuia, umekusanyika ili kuzuia na kupinga jambo Fulani lisifanikiwe, mtu Fulani asifanikiwe kuipokea fursa yake kwa namna yoyote ile, ni watu walio kusanyana kwa lengo moja la kuzuia tu hawana jema wala zuli bali jukumu lao kubwa ni kuzuia tu imeandikwa 1Timotheo 5:15 “Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani”
Kunawatu wengi wanashindwa kuzitumia fursa zao kwa sababu ya umati ulio mbele yao unawazuia. Hivyo kuwa ni watu wa kuhangaika na kuteseka mwaka nenda mwaka rudi, bila mafanikio yoyote hadi kupelekea fursa kuondoka.
N:B yakupasa kutambua fursa ni kama jua linavyo tembea
Maana ya umati
Umati ni mkusanyiko wa watu, vitu, katika eneo moja kwa ajili ya lengo Fulani, inawezekana ikawa ni kikao, kazi, ibaada, tabia, hali, mawazo  au mkutano wa aina yeyote,
Kuzuia maana yake nini
Ni kupinga kitu Fulani au jambo, hali, mawazo, fikira inayoweza kuzuia kitu kisiweze kufanyika/kutendeka kwa wakati unaofaa/sahihi.
Fursa
N i kitu chochote maalumu kilicho mbele yako kwa ajili yako, inawezekana ikawa ni wokovu, biashara, kazi, ndoa au mafanikio yako,
Watu wengi wanateseka ni kwa sababu kuna watu wanaozuia fursa iliyo mbele yao, kwa kuwaona au kutokuwaona kwa macho ya kawaida
Vitu au watu wanaozuia fursa yako  wana weza kuwa  wanaonekana au hawaonekani, wanaoonekana ni wale wanaokupinga wazi wazi kwa kila jambo unalolianzisha na wale wasioonekana wanaweza kukuzuia kwa kutumia njia za kichawi kuzuia usiweze kuipokea fursa iliyo mbele yako au kuzuia wazi wazi.
Imeandikwa Nehemia 4:1-4 “Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba tulikuwa tukiujenga ukuta, akaghadhibika, akaingiwa na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.
 Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je! Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi, nayo yameteketezwa kwa moto?  Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.
Tambua ya kwamba wanaozuia fursa iliyo mbele yako wakawa ni ndugu imeandikwa Mathayo 10:36 “na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”
Ø Inawezekana wakawa  marafiki ulio nao
Ø Inawezekana wakawa  watoto, mume, mke au ndugu mliozaliwa wote
Ø Inawezekana ikawa jamii/washirika/wafanyakazi/viongozi wenzako
Ø Inawezekana ikawa ufahamu wako
Ø Inawezekana ikawa  tabia yako
Ø Inawezekana yakawa mawazo uliyonayo
Ø Inawezekana ikawa  muda
Ø Inawezekana ikawa  imani yako
Ø Inawezekana ikawa  biashara unazozifanya
Ø Inawezekana ikawa kazi unayoifanya
Ø Usipo kuwa makini vinaweza kukuzuia kukutana na fursa iliyo mbele yako,  
Ø Inawezekana vikakuzuia
Ø Kukutana na uponyaji wako
Ø Kuisikia sauti ya Mungu
Ø Kupata msaada
Ø Kufunguliwa
Ø Kukaa miguuni pa Yesu
Ø Kutubu dhambi zako
Ø Kuchelewesha mafanikio yako n.k
Hatua 7 za kuushinda umati unaokuzuia kukutana na fursa iliyo mbele yako
v Kuifahamu kweli juu ya maisha yako imeandikwa Yohana 8:32 ”tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”
v Kuipokea kweli imeandikwa Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
v Mungu awe upande wako imeandikwa warumi 8:31 “Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
v Kumwamini Mungu imeandikwa Waebrania 10:38 “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
v Kuchukua hatua kwa kile unacho kiamini imeandikwa zaburi 37:23-25 “Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, Bwana humshika mkono na kumtegemeza.  Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.
v Kukubali kumsikiliza Mungu ili kupewa maelekezo na njia ya kufanya ili kuwashinda wanaokuzuia kuiona fursa iliyo mbele yako, imeandikwa mithali 16:25 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti”
v Kuwa jasiri juu ya kila jambo la haki Imeandikwa 2Timotheo 1:7 “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi”



HITIMISHO
Watu wanaangamizwa, wanapata shida ni kwa sababu wamekosa maarifa imeandikwa Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”

Umati unaokupinga wewe unaweza ukaja kuwa mateso kwa kizazi chako pia, maombi maalumu yanafanyika hemani ya kutawanya maadui imeandikwa zaburi 68:1 “Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika, Nao wamchukiao huukimbia uso wake”

MIAKA KUMI YA MATESO YA KICHAWI