Wednesday, 3 January 2018

MAISHA BANDIA

UJUMBE EPUKA MAISHA BANDIA,
Yohana 10:10
UTANGULIZI
Kuna watu wengi sana wanateswa kwaajili ya misingi mibovu, iliyojengwa na mababu au wazazi,au wao wenyewe,au na jamii, watu  wanashindwa kuishi maisha halisi waliyokuwa wamekusudiwa na Mungu kishi,ila wanaishi maisha ya kuiga,yaani maisha ya maigizo na ndiyo maisha ya watu wengi nihatari sana kuishi maisha ya kuigiza,

Siku za leo maisha ya watu wengi ni ya kuigiza  
Watu wanaishi maisha ya kuigiza kwasababu maisha yao halisi yalishatekwa na Muovu baada ya kupoteza mahusiano na Mungu, dhambi inampofusha mtu kabisa na kumbadilishia maisha badala ya Nuru anaishi Gizani, dhambi inapoteza kibali cha mtu, hata kama ulikuwa anapendwa namna gani anapotenda dhambi anachukiwa bila sababu,
Maswali ya kujiuliza je mfano wa Mumgu bado unaonekana kwako (umoja) je sura ya Mungu bado inaonekana kwako,(upendo) je uzima wa milele unao (Neno la uzima) je unyenyekevu bado upo,  heshima yako ipo au niyakulazimisha,

TUNAHITAJI UREJESHO  
Mara zote urejesho ni kwa vitu ambavyo vilikua vimehamishwa au vimechukuliwa
 Imeandikwa mwanzo 1:27 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
 
Mungu akaumba mtu Kwa mfano wake, Kwa mfano WA Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.  Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, Na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, Na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Urejesho ni hali ya kurudishwa upya kilichokuwa kimeibiwa au kupotea

Imeandikwa mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda
Kanisa la kristo limeharibiwa na misingi mibovu

Kuna watu wameteswa na hali walizo nazo si kwa sababu hawana fedha, kazi, biashara, mume, au kitu ni kwa sababu wameshindwa kutubu makosa yao (imeandikwa Isaya 40:3-5 Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa; Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.  ,

Imeandikwa Mathayo 3:1-4 “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.  Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu” Yohana 1:23), kumsikiliza Mungu kile anachowaagiza wao kufanya. Mfano kibiblia kunawatu Mungu alisema nao na kuwaagiza wakaweza kumuuliza maswali mengi sana Mungu mfano ukisoma ile
Imeandikwa (Yeremia 1:4-, kutoka 4:1-10-, Yona 1:1-) watu hawa waliweza kujua Nguvu, uweza alizokuwanao Mungu wakaweza kuitii na kuisikiliza Sauti ya Mungu na kuyatenda yale yote Mungu aliyoweza kuwaagiza wao kutenda.
Pia kunawatu wanateswa na hali wanazopitia si kwa sababu hawana pesa, kazi nzuri, ni kwa sababu wamemkataa Mungu (Yohana 1:11)

Kunawatu wanateswa na hali walizo nazo, shida walizo nazo ni kwa sababu wameshindwa kumgeukia Mungu Mazima mazima, mahusiano ya wewe na Mungu yanapoharibika Muovu anachukuwa nafasi kufanya anavyotaka,juu ya maisha yako, na hatoi nafasi ya mtu kutubu atakuongezea tamaa maradufu ili liwe ndilo hitaji lako kuu badala ya hitaji la ufalme wa Mungu mathayo 6:33(ufalme kwanza)ila muovu amewabadilishi fahari ya watu wa leo ni mali,pesa,heshima,mamlaka,ili kufanana na Dunia inavyotaka,

Imeandikwa yakobo 4:1-4. vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!

Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.  Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Watu wanataka vitu vya Mungu lakini hawana haja na Mungu wala hawamuhitaji Wanataka vitu, zaidi kabisa wanamuhitaji Mungu awe kama mlinzi juu ya mali zao imeandikwa Mithali 17:16 Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?

Hadi kupelekea watu kujikuta katika hali kamahi,
o   Kuteswa na mapepo, Vifungo vya nguvu za giza, mizimu, majini.
o   Kuteswa na magonjwa sugu yasio na idadi
o   Kuteswa na matatizo ya ndoa
o   Kuteswa na matatizo ya kifamilia
o   Kukosa kazi
o   Utasa
o   Kuishi maisha ya kutangatanga
o   Biashara kwenda kombo
o   Madeni

-Kama unapitia magumu hayo yote usihofu endelea kujifunza na kufuatilia somo hili kwani:
Tumaini lako bado lipo haina budi kukata tama, haijalishi umewahi kushindwa mara ngapi, na wapi,  na kwa nini Yesu kristo alizaliwa kimiujiza ili aje kutenda miujiza, majibu ya shida zako unamuhitaji Yesu kristo aingie ndani ya maisha yako, akuongoze, juu ya yote uyafanyayo,

Ufanye nini sasa ili uweze kurejeshwa upya na Mungu
Ili kulejezwa upya Mungu anahitaji utayari wako juu ya yake, na kuweza kuzikataa hali zote unazozipitia, au   ulizowahi kuzipitia katika maisha yako kwa kumruhusu Roho mtaakatifu aingie ndani yako na kuishi na wewe na kukutangulia kwa kila jambo ndipo utaweza kufanya na kuzifuata hatua zifuatazo zinazokuhitaji 

uzifanye ili uweze kurejezwa upya na Mungu.
ü Kuwa mtu wa toba na msamaha
ü Kujitahidi kumsikiliza Mungu
ü Kuwa mtendaji wa neon la Mungu
ü Kumkubali Mungu aishi ndani yako (Yohana 1:12)
ü Kuitii sauti ya Mungu  (Isaya 1:19)
ü Kukubali kuhamishwa na Mungu (Wakolosai 1:13)

FAIDA ZA KUREJESHWA UPYA NA MUNGU

v Kuimarishwa kiuchumi, familia, ndoa, biashara, masomo na kazi,
v Kuwa na uzima tele
v Hakuna utasa tena katika maisha yako,
v Kustawi (kutoka 23:20-)
v Kuokolewa na Mungu (Yeremia 15:21 Isaya 38:6)
v Kushinda
v Hakuna maadui na  mateso kamwe juu yako (Kutoka 23:22-
v Kuwa na utiisho wa KIMUNGU
v Kuongezewa miaka ya kuishi (Isaya 38:1-)
v Kuendelea mbele (kutoka 15:14)
v Mungu kujipatia utukufu kwa maadui zetu (Kutoka 14:18)
v Kupitishwa katika vizuizi (Kutoka 14:16)
v Kuwa kinywa cha Mungu

Imeandikwa Kumbukumbu 6:5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.  Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;  nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
Imeandikwa Yakobo 4:44 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Imeandikwa Galatia 4:19 Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu;
Imeandikwa Warumi 8:29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.

Imeandikwa Mithali 28:13. Afichaye dhambi zake hatafanikiwa bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”
Hitimisho maombi ya toba
Imeandikwa Yeremia 9:23
Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;

bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana,



Imeandaliwa na MTU WA MUNGU BABA NABII SAMSON MBOYA WA HUDUMA YA HEMA YA KINABII TANZANIA-BONDE LA UZIMA NYANKUMBU GEITA

MIAKA KUMI YA MATESO YA KICHAWI