wana wa Manabii Ndani ya Hema ya Kinabii wakiomba maombi ya kupinga Roho ya Mauti,
somo; NI KUPINGA ROHO YA MAUTI
2Wafalme 4:40
Utangulizi:si kila Kifo ni Mupango wa Mungu, vingine ni Mipango ya wanadamu,lazima ipingwe katika Jina la Yesu.
Mauti
inaweza kujificha sehemu ya aina yeyote ile maana ni roho isiyoonekana kirahisi
inaweza kuuwa kiumbe, kitu, au jambo flani, husika, lililolengwa kuuwawa,
ambavyo inahitaji macho ya rohoni kuiona na kuiondoa, pia kunahitajika nguvu za
Rohoni,
Mauti
ni Nguvu ya Uharibifu,inayoweza kuingia katika
kiumbe, kitu, au mazingira wakati wowote kwa yeyote kwa chochote kwaajili ya
kuuwa, ndiyo maana inaitwa jina la mauti,
Mara nyingi mauti inaanzia roho japo matokeo
ni mwili, baada ya kuona viashiria ndipo utasikia vilio leo Mungu anataka
kukusaidia
Roho
ya mauti inaweza kumtesa mtu kwaajili ya,
Mfano:
§
Ufahamu kutokuwa na taarifa
sahihi inaweza kukusababishia kifo
§
Roho ambayo hainaulizi wa
roho wa bwana,
§
Jamii iliyokuzunguka yaani
washauri wakiwa hawana ufahamu matokeo
§
Mazingira yaliyokuzunguka
yanaweza kukusababishia mauti
§
Tabia inaweza kuruhusu mauti
ndani yako
§
Kukosa nguvu ya kiroho ndani
yako,(Elisha alikuwa rohoni,
Isaya 42:2 watu wanaweza kuibiwa wao au roho
zao kupitia uchawi Kuna majini au majoka ambayo yanaingia ndani ya mwili wa mtu
na kuitoa roho yake. Haya ukipeleka hospitali si rahisi kuona katika vipimo
vyao Hospitali wanaweza kupima macho, punzi, na mzunguko wa damu,mfumo wa
hewa,viungo mfumo wa akili, kama vinafanya kazi na kama havifanyi kazi jibu wanasema kiungo kimekufa au mtu
mwenyewe.
Watu waliyoiona mauti ndani ya sufuria,
“Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu waMunguWala hawakuweza kula.” 2Wafalme 4:40
“Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu waMunguWala hawakuweza kula.” 2Wafalme 4:40
Maombi
ya elsha kupinga roho ya mauti
Kama mauti ipo ndani ya sufuria basi kumbe mauti inaweza kuwa ndani ya gari yako,mauti inaweza kuwepo ndani ya nyumba yako,mauti inaweza kuwa ndani ndoa,shamba lako,Biashara yako,inaweza kuingia katika Huduma yako ikafa, inaweza pia kuagizwa popote kwa yeyote wakati wowote, kifo ni uharibifu,au ni utengano na kinaweza kumtenga mtu na familia yake,

Kinaweza kutenganisha ndoa, kinaweza kumtenga
mtu na kazi yake. Kinaweza kumfuata mtu kikamuingia na kumtenganisha na mwili
wake au kumtenganisha na jambo lolote alilo nalo.
Dalili ya Mtu mwenye roho ya mauti,
§
Anaandamwa na majanga kila namna yasiyoeleweka chanzo nini
§
Kila analoanzisha hata kama
ni zuri kiasi gani lazima life au liishie njiani
§
Ni mtu wa kufanya maamuzi ya
haraka na baadayekujutia maamuzi yake
§
Ni mtu wakupuuzia kila jambo
analoshauriwa,
§
Ni mtu mwenyekiburi kikubwa
sana
§
Ni mtu wa kujitenga tenga na
wenzake
§
NI mtu wa kushambuliwa na
magonjwa yasiyoeleweka
§
Ni mtu wa kuandamwa na ajali
zinazoandamana kwa msimu flani
§
Ni mtu asiyekuwa na makazi
ni wa kuhama hama ovyo,
§
Ni mtu anayedhufika na
wakati mwingine haumwi
Waliowahi
kuona roho ya Mauti,
“Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya
kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye.
Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa
tauni na kwa hayawani wa nchi. Imeandikwa Ufunuowa Yohana 6:8~10
kwa kuwa kifo ni roho Basi roho chafu zinaweza kutumia mauti kukumaliza mapepo, majoka, mizimu, majini na miungu. Kifo hakina macho lakini hakikosei kifo hakina kichwa ila kina kina akili kinaweza kujua kule kilikotumwa na kujuwa kunanaendeka au hakuendeki mauti inaweza kuishi na Mtu kwa muda mrefu kabisa isipoondolewa basi inamaliza kazi,

ya Hezekia kupinga roho ya mauti
Imeandikwa,Isaya38:1-7Hezekia tayari mauti ilisha ingia ndani na chanzo
kilisha patikana ilikuwa inangoja muda wa kumaliza kazi ya kumuuwa ezekia,
Kwa mfano anayejifika mabomu, tunasema mauti
ndani ya mtu,anayetoa mimba,anayepiga mke,au mme,anayetumia madawa ya
kulevya,anayechokoza wengine,anayedhulumu pesa ya mwenzake,anayezini na mke
asiye mke wake,anayefanya uasherati,anayeiba,chochote cha mtu,iwe pesa au mke,
Kifo kinaweza kuwekwa kwenye gari.kikaishi Kwa
muda kusubiri chanzo au sababisho ili kuuwa.
Kuna mapepo yanayoweza kuitwa na wachawi, na kuagizwa kuleta mauti katika maisha ya mtu aliyekusudiwa niliwahi kufundisha alama za mapepo maringo,kupita kawaida , ukahaba, kuharibu mimba, kuvunja ndoa, kusababisha utasa,ajali zisizoeleweka vyanzo na mambo mengine. Kuna majini/mapepo ya uchizi, kuna mashetani maalum yanayotenda kazi kulingana na ngazi zao na maagizo. Mapepo yanayosumbuwa Huduma ni tofauti na la biashara,
Si kila maombi yanajibiwa kirahisi tu,
“Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.” Imeandikwa Daniel 10:13
Kuna majini ya aina Fulani ambayo yanatumwa kwenda kumwingia mtu na kukaa ndani yake kusubiri tarehe iliyopangwa ili kutenda kazi iliyokusudiwa.

Kifo
kilikuwa ndani ya sufuria kinangoja watu wale chakula ili wafe,
Kifo kilikuwa ndani ya sufuria kinasubiri
watu wale lakini kikateguliwa na Mtu wa Mungu Elsha hii inadhihirisha kuwa watu
wengi wanatembea na kifo ndani yao bila ya wao kujua. Unaweza kuona kwamba mtu
anaona hatari iko mbele yake lakini anaenda bila kuiona kwasababu kifo kiko
ndani yake kimempofusha macho asiione na kinasubiri nafasi ili kimtenganishe na
mwili wake.
Kila unayemwona hapa duniani anatumikia utawala wa juu au wa chini kwa kujua au bila ya yeye kujua.
Inawezekana rafiki yako wa kazini anakuonea wivu jinsi unavyofanikiwa akakuendea kwa mganga wa kienyeji ili ufe umuachie nafasi uliyo nayo. Akifika anapewa masharti na Yule mganga anatuma kifo kuja kwako. Kifo kinaweza kutumwa kwa mtu kulingana na mazingira aliyo nayo.

Mapepo hayapendi kutambuliwa kujulikana
hutengeneza mazingira ambayo watu wakiangalia watasema marehemu alifariki kwa
ajali, kwa kuugua, kwa presha na watu wakiangalia wanakubaliana na hali hiyo
kumbe ni kifo kimemchukua mtu huyo.
Roho ya mtu inaweza kutolewa na joka au jini
ambalo linakuja kuingia ndani ya mtu kuitoa roho ya mtu. Kwasababu roho ndiyo
imtiayo mwili uzima kwahiyo roho ya mtu ikitolewa nje ya mwili, mtu huyo
unaacha kufanya kazi. Mtu huyo anaitwa amekufa, marehemu
Mauti
ikiwa mahali jina linabadilika kwa mtu anaitwa maiti,au marehem ndani ya mji
utaitwa Mji wa mauti unaitwa mji wa mauti kwa sababu kazi yake kubwa ni
kusababisha mauti.
2WAFALME
2:19 “watu wa mjini wakamwambia Elisha, angalia twakusihi, mahali pa mji huu ni
pazuri kama bwana wangu aonavyo, lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa
mapoza”. Unaweza ukawa unafanya biashara Fulani na unaweza ukawa unapata faida
lakini kumbe ndani ya biashara hiyo kuna mauti. Kwa mfano: biashara ya
bodaboda, watu wanasema “asante mchina ametusaidia” lakini angalia jinsi
ambavyo watu wengi wanakufa kutokana na hizo bodaboda. Katika ndoa watu
wanajifunguwa wanakufa ovyo, mitaa mingine uwezi kusikia harusi hata siku moja
utasikia taarifa za msiba tu, kuna mtaa kila biashara inayoanzishwa lazima ife
maana mauti ipo ndani ya mtaa,
Pata maarifa leo na uanze mapambano
“Kwa mamlaka ya jina la Yesu kila roho ya
mwanadamu, mashetani, kifo, na mapepo yote na miungu yote ya mauti kokote kwa yeyote palipowekwa roho ya mauti iliyotumwa
kuja kuingia ndani yangu, kwenye biashara yangu, kwenye kazi yangu,uchumba,ndoa,mashamba,
ili nife zife,au kazi yangu ife ninaondoa kwa jina la Yesu, ninazifunga na
kuzivunja roho zote zilizotumwa kwangu kwamamlaka ya jina la Yesu. Amen”
wakala
wa kerubi anaweza kutuma roho ya mauti ikakutesa hadi kifo,
Bwana
MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote
vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu;
je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na
kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa
ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao
haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa
kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. Basi Bwana MUNGU asema hivi;
Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za
watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami
nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.” Ezekiel 13:18~20